Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 11, Sehemu 2 · Art. 181

Kuondolewa kwa gavana wa kaunti

  • Gavana wa kaunti anaweza kuondolewa kwa ukiukaji mkubwa wa Katiba au sheria, kosa zito, matumizi mabaya ya ofisi au maovu makubwa, au kutokuwa na uwezo wa kimwili au kiakili.
    Art. 181(1)

    (1) Gavana wa kaunti anaweza kuondolewa kutoka afisini katika msingi wowote kati ya misingi ifuatayo- (a) ukiukaji wa katiba hii au sheria yoyote uliokithiri ; (b) ikiwa pana sababu ya kutosha kuamini kuwa gavana huyo wa kaunti amefanya uhalifu chini ya sheria ya taifa au kimataifa; (c) kutumia mamlaka ya afisi vibaya au utovu wa nidhamu uliokithiri; (d) kukosa uwezo wa kimwili au kiakili kutekeleza majukumu ya afisi ya gavana.

    Soma kifungu kamili →
  • Bunge lazima liweke utaratibu wa kuondolewa.
    Art. 181(2)

    (2) Bunge litatunga sheria ya kutoa kanuni za kufuatwa kumuondoa gavana afisini kwa msingi wowote uliotajwa katika ibara ya (1).

    Soma kifungu kamili →

Soma nakala halisi →

    Tafuta →