Sura 11, Sehemu 6 · Art. 192
Kusimamishwa kwa muda kwa serikali ya kaunti
- Rais anaweza kusimamisha serikali ya kaunti katika dharura inayotokana na mzozo wa ndani au vita, au katika mazingira mengine ya kipekee.
Art. 192(1)
(1) Rais anaweza kusimamisha serikali ya kaunti kwa muda- (a) wakati wa dharura inayotokana na mizozo ya ndani au vita; au (b) wakati wa hali za kipekee zinazohitaji kuchukuliwa kwa hatua kama hiyo.
Soma kifungu kamili → - Kusimamisha katika mazingira ya kipekee kunahitaji tume huru ya uchunguzi, kuridhika kwa Rais, na idhini ya Seneti.
Art. 192(2)
(2) Serikali ya kaunti haitasimamishwa kwa muda kulingana na ibara ya (1) (b) hadi tume huru ifanye uchunguzi wa mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake, Rais wa taifa aridhike kwamba mashtaka ni ya haki na seneti imeyaidhinisha.
Soma kifungu kamili → - Kusimamishwa hakuwezi kuzidi siku 90, kisha uchaguzi hufanyika.
Art. 192(5)
(5) kusimamishwa kwa muda katika kifungu hiki hakuwezi kuwa kwa zaidi ya siku tisini.
Soma kifungu kamili →
- Serikali ya kaunti inaweza kusimamishwa katika hali mbaya sana tu, na kwa muda mfupi.
Art. 192(1)
(1) Rais anaweza kusimamisha serikali ya kaunti kwa muda- (a) wakati wa dharura inayotokana na mizozo ya ndani au vita; au (b) wakati wa hali za kipekee zinazohitaji kuchukuliwa kwa hatua kama hiyo.
Soma kifungu kamili →