Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 13, Sehemu 2 · Art. 233

Tume ya Huduma za Umma

  • Kuna Tume ya Huduma za Umma, inayoundwa na mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wengine saba walioteuliwa na Rais kwa idhini ya Bunge la Kitaifa.
    Art. 233(2)

    (2) Tume ya Huduma za Umma inahusisha mwenyekiti, naibu wa mwenyekiti na wanachama wengine saba walioteuliwa na Rais na kuidhinishwa na Baraza Kuu la Kitaifa.

    Soma kifungu kamili →
  • Mjumbe hapaswi kuwa ameshikilia ofisi ya kisiasa au kiti cha ubunge katika miaka mitano iliyopita.
    Art. 233(3)

    (3) Kwa mujibu wa ibara ya (4), mtu hastahili kuteuliwa kama mwanachama wa Tume hii iwapo mtu huyo- (a) kwa kipindi cha miaka mitano iliyotangulia alikuwa na afisi au amewania kiti katika uchaguzi kama- (i) mwanachama wa bunge au wa baraza la kaunti; au (ii) mwanachama katika bodi ya uongozi ya chama cha kisiasa; au (b) ana wadhifa katika afisi yoyote ya serikali; (c) anagombea kiti, au kwa wakati wowote amewahi kugombea kiti cha ubunge au katika baraza la kaunti; au (d) anashikilia, au kwa wakati wowote ule, amewahi kushikilia kiti cha afisi ya shirika la kisiasa linalofadhili au kuunga mkono mgombeaji wa ubunge au wa baraza la kaunti.

    Soma kifungu kamili →

Soma nakala halisi →

    Tafuta →