Sura 15 · Art. 251
Kuondolewa afisini
- Mjumbe wa tume au mshikiliaji wa ofisi huru anaweza kuondolewa tu kwa ukiukaji mkubwa wa Katiba au sheria, maovu makubwa, kutokuwa na uwezo, kukosa umahiri, au kufilisika.
Art. 251(1)
(1) Mwanachama wa Tume (isipokuwa aliye mwanachama kutokana na wadhifa wake) , au anayeshikilia wadhifa wa afisi huru, anaweza kuondolewa afisini kwa sababu ya- (a) ukiukaji uliokithiri wa Katiba hii au sheria yoyote ikiwa ni pamoja na kuvunja sheria katika sura ya sita; (b) utovu wa nidhamu ama ni katika utendakazi wa mwanachama au yule anayeshikilia wadhifa wa afisi huru; (c) kutokuwa na uwezo wa kimwili au kiakili katika kutekeleza majukumu ya kiafisi; (d) kushindwa kufanya kazi; au (e) kufilisika.
Soma kifungu kamili → - Mtu anaweza kuwasilisha ombi kwa Bunge la Kitaifa, ambalo linaweza kulipeleka kwa Rais, ambaye huteua kamati kuchunguza.
Art. 251(2)
(2) Mtu anayeazimia kuondolewa kwa mwanachama wa tume au anayeshikilia wadhifa wa afisi huru kwa misingi yoyote iliyotajwa katika ibara ya (1) anaweza kuwasilisha malalamiko kwa Baraza la Bunge huku akifafanua yale yote yanayothibitisha azma hiyo.
Soma kifungu kamili →
- Kamishna anaweza kuondolewa kwa sababu kubwa tu, baada ya uchunguzi.