Art. 10
Maadili ya kitaifa na kanuni za utawala
- Viongozi lazima wawe wa haki, waaminifu na wawajumuishe wote wanapofanya maamuzi.
Art. 10(2)
(2) Maadili ya kanuni za uongozi ni pamoja na – (a) Uzalendo, umoja wa kitaifa, kushirikiana na ugatuzi wa mamlaka, utawala wa sheria, demokrasia na kushiriki kwa watu; (b) heshima ya binadamu, usawa, haki za jamii, kushirikishwa, haki za binadamu, kutobagua na kulindwa kwa makundi yaliyotengwa. (c) utawala mwema, uadilifu, uwazi na uwajibikaji; na (d) maendeleo endelevu.
Soma kifungu kamili →