Art. 18
Sheria kuhusu Uraia
- Bunge hutungasheria kuhusu kuwa raia na kuhusu kubaki Kenya.
Art. 18(a)
Bunge litaunda sheria — (a) kueleza taratibu ambazo kupitia kwazo mtu anaweza kuwa raia; (b) kuongoza uingiaji na kukaa nchini Kenya (c) kutoa hali ya wakaazi wa kudumu; (d) kutoa nafasi ya kukana uraia kwa hiari; (e) kutoa taratibu za kupokonywa uraia; (f) kuamua majukumu na haki za raia; na (g) Kwa jumla, kuyawezesha masharti ya Sura hii.
Soma kifungu kamili →