Art. 32
Uhuru wa dhamiri, dini, imani na maoni
- Unaweza kuamini unachoamini, na kufuata dini yako, peke yako au pamoja na wengine.
Art. 32(1)
(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kuwa na msimamo, dini, mawazo, imani na maoni.
Soma kifungu kamili → - Hakuna anayeweza kukuzuia kwa sababu ya dini yako.
Art. 32(3)
(3) Mtu hatazuiwa kuingia ama kujiunga na taasisi yoyote, kunyimwa ajira au kufika mahali fulani au kufurahia haki yoyote kwa sababu ya imani yake ya kidini.
Soma kifungu kamili →