Art. 53
Watoto
- Kila mtoto anapaswa kuwa na jina, kwenda shule, na kuwa na chakula, nyumba na daktari.
Art. 53(1)
(1) Kila mtoto ana haki ya- (a) jina na uraia kuanzia anapozaliwa; (b) elimu ya msingi bila malipo na ya lazima; (c) Lishe bora ya kimsingi, makazi na huduma za afya ; (d) kulindwa dhidi ya kutumiwa vibaya, kutelekezwa, tamaduni za kuumiza, aina zozote za ghasia, matendo na adhabu zisizo za kibinadamu, kutumiwa vibaya, na kazi yoyote ya kunyanyasa au ya kuhatarisha; (e) kutunzwa na kulindwa na wazazi, ambayo inahusu wajibu sawa kutoka kwa mama na baba wa kumkimu mtoto, iwe wameoana au la; na (f) kutofungwa kinyume na matakwa yake isipokuwa endapo hiyo ndiyo hatua ya mwisho, na wakizuiliwa- (i) kuzuiliwa kwa muda mfupi na unaostahili tu; na (ii) kutenganishwa na watu wazima katika jela huku ikizingatiwa umri na jinsia ya mtoto.
Soma kifungu kamili → - Jambo la muhimu zaidi ni lile lililo bora kwa mtoto.
Art. 53(2)
(2) maslahi ya mtoto ni muhimu sana katika kila suala linalomhusu mtoto.
Soma kifungu kamili →