Art. 55
Vijana
- Vijana wanapaswa kuweza kujifunza, kupata kazi, na kushiriki katika maamuzi.
Art. 55
(1) Serikali itachukua hatua, ikiwemo miradi ya vitendo sawazishi, kuhakikisha kwamba vijana- (a) wanapata elimu na mafunzo yanayofaa; (b) wana fursa ya kujumuika, kuwakilishwa na kushiriki katika nyanja za kisiasa, kijamii kiuchumi na nyanja nyingine za maisha; (c) wanapata kazi; na (d) kulindwa dhidi ya tamaduni zinazodhuru na kunyanyasa.
Soma kifungu kamili →