Art. 80
Sheria kuhusu uongozi
- Bunge hutungakanuni na adhabu zinazowafanya viongozi kuwa waaminifu.
Art. 80
Bunge litatunga sheria – (a) kubuni taratibu na mikakati ya kutekeleza sura hii kwa njia ifaayo; (b) kupendekeza adhabu zaidi ya zile zinazotajwa katika Kifungu cha 75, ambazo zinaweza kuamriwa kwa sababu ya kutofuata maagizo ya Sura hii; (c) kusaidia katika utekelezaji wa Sura hii pakiwa na marekebisho yanayofaa kwa maafisa wa umma; na (d) kuunda masharti mengine yoyote katika kuhakikisha udumishaji wa kanuni za uongozi na uadilifu ambayo yametajwa katika Sura hii, na utekelezaji wa masharti ya Sura hii.
Soma kifungu kamili →