Art. 86
Upigaji kura
- Kura lazima zihesabiwe kwa makini na matokeo yaambiwe kila mtu haraka.
Art. 86(b)
Katika kila uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itahakikisha kwamba- (a) katika njia yoyote ya upigaji kura itakayotumiwa, mfumo unakuwa rahisi, sahihi, wa kuthibitika, salama, unaowajibika na ulio na uwazi; (b) kura zinazopigwa zinahesabiwa, kuorodheshwa na matokeo kutangazwa moja kwa moja na afisa msimamizi wa kituo cha upigaji kura hapo kituoni; (c) matokeo kutoka kwa vituo vingine vya upigaji kura yanajumlishwa kwa uwazi na kutangazwa moja kwa moja na afisa msimamizi wa kituo cha upigaji kura; na miundo na taratibu mwafaka zimewekwa ili kuondoa uwezekano wa kuhusishwa kwa mienendo yoyote mibaya, ukiwemo uhifadhi salama wa vifaa vya uchaguzi.
Soma kifungu kamili →