Art. 98
Uanachama wa Seneti
- Seneti ina mjumbe mmoja aliyechaguliwa kwa kila kaunti kati ya 47, pamoja na wengine.
Art. 98(1)
(1) Seneti itajumuisha- (a) wanachama arobaini na saba, kila mmoja wao akiwa amechaguliwa na wapigakura waliosajiliwa kwenye kaunti, na kila kaunti ikiwa ni eneowakilishi la mwanachama mmoja; (b) wanachama wanawake kumi na sita watakaoteuliwa na vyama vya kisiasa kulingana na usawa wao wa wanachama kwenye Seneti waliochaguliwa chini ya ibara ya (a) kwa mujibu wa Kifungu cha 90; (c) wanachama wawili wakiwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja ili kuwakilisha vijana; (d) wanachama wawili wakiwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja wakiwakilisha watu wenye ulemavu; na (e) Spika atakayekuwa mwanachama m’badala kwa mujibu wa wadhifa wake.
Soma kifungu kamili →