Art. 118
Kufikiwa na kushiriki wa umma
- Bunge hukutana hadharani, na watu wanaweza kushiriki.
Art. 118(1)
(1) Bunge- (a) litafanya shughuli zake kwa njia ya uwazi, na kufanya vikao vyake na vile vya kamati zake mbele ya umma; na (b) litarahisisha kushiriki na kuhusishwa kwa umma katika shughuli za kutunga sheria na shughuli nyingine za Bunge na kamati zake.
Soma kifungu kamili →