Art. 134
Matumizi ya mamlaka ya Urais kwa Rais wa muda
- Wakati hakuna Rais kamili, mamlaka mengine makubwa hayawezi kutumika.
Art. 134(1)
(1) Yeyote anayeshikilia afisi ya Rais au yule ambaye anayeidhinishwa kwa mujibu wa Katiba hii kutumia mamlaka ya Rais- (a) Katika kipindi kinachoanzia mnamo tarehe ya kwanza kwenye uchaguzi wa Rais, na kukamilika wakati Rais mpya anapochukua hatamu za afisi; au (b) wakati Rais hayupo au, hawezi kutekeleza mamlaka yake au wakati mwingine kama ilivyoelekezwa katika kifungu cha 147 (3), hawezi kutekeleza mamlaka ya Rais yaliyotajwa katika ibara ya ya (2).
Soma kifungu kamili →