Art. 149
Nafasi ya kazi katika afisi ya Naibu wa rais
- Kama Naibu wa Rais anaondoka, Rais huchagua mwingine na Bunge huthibitisha.
Art. 149(1)
(1) katika muda wa siku kumi na nne baada ya kutokea nafasi ya kazi katika afisi ya Naibu wa rais, Rais atamteua mtu mwingine kujaza nafasi hiyo, nalo Baraza la Kitaifa litapiga kura ya uamuzi wa uteuzi huo katika muda wa siku sitini baada ya kuupokea.
Soma kifungu kamili →