Art. 159
Mamlaka ya Mahakama
- Mahakama huamua kesi kwa haki, na kila mtu ni sawa mbele yao.
Art. 159(2)
(2) Katika kutekeleza majukumu ya kimahakama, mahakama na mahakama maalum zitaongozwa na kanuni zifuatazo- (a) haki itatendwa kwa kila mtu bila kuzingatia hadhi ; (b) Haki haitacheleweshwa; (c) njia m’badala za kusuluhisha kesi zikiwemo msamaha, mashauriano, na maridhiano na njia za kitamaduni za kusuluhisha migogoro zitaimarishwa, kwa mujibu wa ibara ya (3); (d) haki itatolewa kwa kuzingatia matatizo yaliyopo ya utaratibu wa kitaalamu; na (e) lengo na kanuni za Katiba hii zitatunzwa na kuendelezwa.
Soma kifungu kamili →