Art. 168
Kuondolewa kutoka afisini
- Jaji anaweza kuondolewa kwa sababu kubwa tu, kwa mchakato maalum.
Art. 168(1)
(1) Jaji wa mahakama yenye mamlaka ya juu anaweza kuondolewa tu kutoka afisini kwa misingi ya – (a) kushindwa kutekeleza majukumu ya afisi kwa sababu ya ukosefu wa uwezo wa kimwili au kiakili; (b) kukiuka kanuni za utendakazi zilizowekewa majaji wa Mahakama Makuu kupitia Sheria ya Bunge. (c) kufilisika; (d) kutokuwa na umilisi; au (e) utovu wa nidhamu, ama katika utekelezaji wa majukumu ya jaji au vinginevyo.
Soma kifungu kamili →