Art. 175
Kanuni za Serikali ya ugatuzi
- Serikali za kaunti lazima ziwe za kidemokrasia na ziwe na fedha za kutosha kuwahudumia watu.
Art. 175(a)
Serikali za kaunti zilizobuniwa chini ya Katiba hii zitazingatia kanuni zifuatazo- (a) Serikali za kaunti zitazingatia misingi ya kidemokrasia na utengano wa mamlaka. (b) Serikali za kaunti sharti ziwe na njia za kuaminika za kuzalisha mapato ili kuziwezesha kuendesha shughuli zao na kutoa huduma kwa njia bora; na (c) isiyo zaidi ya theluthi mbili ya wanachama wawakilishi wa taasisi za umma katika Serikali za kaunti watakuwa wa jinsia moja.
Soma kifungu kamili →