Art. 183
Majukumu ya mamlaka kuu za kaunti
- Kamati kuu ya kaunti hutekeleza sheria za kaunti na kuendesha huduma za kaunti.
Art. 183(1)
(1) Kamati kuu ya kaunti ina majukumu yafuatayo: (a) utekelezaji wa sheria za bunge la kaunti; (b) utekelezaji, katika kaunti , sheria za taifa inavyohitajika kisheria; (c) kusimamia shughuli za utawala wa kaunti na idara zake; na (d) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Katiba hii na sheria ya nchi.
Soma kifungu kamili →