Art. 187
Kuhamisha mamlaka na majukumu kati ya viwango vya serikali
- Serikali zinaweza kukubaliana kugawana baadhi ya kazi, na fedha zake zinahama pia.
Art. 187(1)
(1) Mamlaka au majukumu ya Serikali katika kiwango kimoja yaweza kuhamishwa hadi kiwango kingine cha Serikali kwa makubaliano kati ya Serikali hizo mbili kama- (a) mamlaka au jukumu hilo litapata uzito zaidi likitekelezwa na Serikali hiyo itakayolichukua; na (b) kuhamishwa kwa mamlaka au majukumu kunaafikiana na sheria ambazo zinafungamana na utekelezaji wake.
Soma kifungu kamili →