Art. 189
Ushirikiano wa Serikali ya kitaifa na za kaunti
- Serikali ya kitaifa na za kaunti lazima zifanye kazi pamoja na kutatua kutokuelewana kwa amani.
Art. 189(1)
(1) Serikali katika viwango vyovyote- (a) itaendesha na kutumia mamlaka yake ikiheshimu utekelezaji na heshima za taasisi nyinginezo za viwango vingine za Serikali na kuheshimu hadhi ya kikatiba na taasisi za serikali katika viwango vingine, na kwa serikali ya kaunti, katika kiwango cha kaunti; (b) kusaidia, kushirikiana na kushauriana na Serikali katika viwango vyote vifaavyo, kutekeleza sheria katika viwango vyote vya Serikali; na (c) kushauriana na Serikali katika ngazi tofauti tofauti kwa minajili ya kubadilishana mawazo, kusimamia sera na utawala, huku uwezo ukikuzwa.
Soma kifungu kamili →