Art. 191
Mkinzano wa sheria
- Sheria za kitaifa na za kaunti zikigongana, kuna kanuni zinazoamua ipi inatumika.
Art. 191(2)
(2) Sheria ya kitaifa itakuwa na mamlaka juu ya ile sheria ya kaunti iwapo- (a) sheria za kitaifa zitatumika kwa usawa katika Kenya nzima na masharti mengine yaliyomo katika ibara ya (3) yametoshelezwa; au (b) sheria za kitaifa zinalenga kudhibiti maamuzi yasiyo ya busara ya kaunti ambayo- (i) yanaweza kuwa na athari mbaya kiuchumi, kiafya ama maslahi ya usalama wa Kenya au kaunti nyingine; au (ii) zitazuia utekelezaji wa sera za uchumi wa kitaifa.
Soma kifungu kamili →