Art. 193
Sifa za wagombea uanachama wa baraza la kaunti
- Ili kuwa MCA, lazima uwe mpiga kura aliyejiandikisha na ukidhi masharti.
Art. 193(1)
(1) Labda azuiwe na ibara ya (2), mtu atahitimu kugombea uanachama katika baraza la kaunti kama- (a) amesajiliwa kama mpiga kura; (b) anatimiza mahitaji yote ya kielimu, tabia nzuri na maadili mema kama inavyotakikana kwa mujibu wa Katiba au Sheria ya Bunge; na (c) ama- (i) ameteuliwa na chama cha kisiasa; au (ii) ni mgombeaji wa kujitegemea aliyeungwa mkono na watu mia tano waliosajiliwa kama wapiga kura katika wadi husika.
Soma kifungu kamili →