Art. 194
Kuondoka afisini kama mwanachama wa baraza la kaunti
- Kiti cha MCA kinakuwa tupu kama akifa, akijiuzulu, au akiacha kufuata kanuni.
Art. 194(1)
(1) Afisi ya mbunge wa baraza unge la kaunti huwa wazi kutokana na- (a) iwapo mbunge atafariki; (b) kama mbunge atakosa vikao vinane vya bunge bila idhini iliyoandikwa kwa spika wa bunge, na hawezi kutoa sababu za kutosha za kutohudhuria vikao hivyo; (c) kama mtu huyo ataondolewa afisini kwa mujibu wa Katiba hii au kwa mujibu wa sheria ya kifungu cha 80. (d) mbunge akijiuzulu kwa kumwandikia spika wa bunge; (e) iwapo baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge- (i) kama mwanachama wa chama cha kisiasa atajiuzulu, ama ikichukuliwa amejiuzulu kutoka kwa chama kwa mujibu wa sheria inayotajwa katika Ibara ya (2); au (ii) baada ya kuchaguliwa bungeni kama mgombea huru, anajiunga na chama cha kisiasa (f) kukamilika kwa kipindi cha bunge; au (g) kama mwanachama ataondolewa afisini kwa misingi ya uchaguzi ilivyowekwa katika Kifungu cha 193 (2).
Soma kifungu kamili →