Art. 196
Kushiriki kwa umma, mamlaka, haki na kinga kwa baraza la kaunti
- Mabunge ya kaunti hukutana hadharani, na watu wanaweza kushiriki.
Art. 196(1)
(1) Baraza la kaunti – (a) litaendesha shughuli zake kwa uwazi, na kufanya vikao vyake na vile vya kamati zake mbele ya umma; na (b) kuhimiza watu kushiriki katika kutunga sheria na katikacshughuli nyingine za baraza na kamati zake.
Soma kifungu kamili →