Art. 252
Majukumu na Mamlaka ya jumla
- Tume zinaweza kuchunguza malalamiko na kusaidia kutatua migogoro.
Art. 252(1)
(1) Kila tume, na anayeshikilia wadhifa wa afisi huru – (a) anaweza kuchukua hatua ya kufanya uchunguzi au kufuatia malalamiko yaliyotolewa na mwananchi; (b) ana mamlaka muhimu ya kupatanisha , kusuluhisha na kujadiliana ili kupata maafikiano; (c) itaajiri wafanyakazi wake; na (d) inaweza kutekeleza majukumu na mamlaka mengine yoyote iliyopewa na sheria, mbali na majukumu na mamlaka iliyopewa na Katiba hii.
Soma kifungu kamili →