Art. 256
Marekebisho yanayotokana na juhudi za Bunge
- Bunge linaweza kubadilisha Katiba, lakini linahitaji wingi mkubwa na lazima liruhusu umma kujadili.
Art. 256(1)
(1) Mswada wa kurekebisha Katiba hii – (a) unaweza kuwasilishwa katika mojawapo ya viwango vya Bunge; (b) haupaswi kuangazia suala lolote jingine isipokuwa yale yanayotokana na marekebisho ya sheria katika Mswada huo; (c ) hautafikishwa kusomwa kwa mara ya pili katika mojawapo ya vitengo vya Bunge, katika muda wa siku tisini baada ya kusomwa kwa Mswada kwa mara ya kwanza katika Bunge hilo; na (d) utakuwa umepitishwa na Bunge wakati kila mojawapo ya vitengo vya Bunge kimepitisha Mswada huo katika kusomwa kwa mara ya pili na tatu, kwa idadi isiyopungua thuluthi mbili ya wabunge wote katika ngazi hiyo.
Soma kifungu kamili →