Art. 110
Miswada kuhusu Serikali za Kaunti
- Miswada mingine huathiri kaunti, na Bunge huamua jinsi ya kuishughulikia.
Art. 110(1)
(1) Katika Katiba hii, ‘Mswada unaohusu serikali ya kaunti unamaanisha’- (a) mswada ulio na masharti yanayoathiri majukumu na mamlaka ya serikali za kaunti zilizotajwa katika Mpangilio wa Nne; na (b) Mswada unaohusiana na uchaguzi wa mwanachama wa bunge la kaunti au serikali za kaunti. (c ) mswada uliotajwa katika Sura ya Kumi na mbili unaoathiri fedha za serikali za kaunti.
Soma kifungu kamili →