Art. 181
Kuondolewa kwa gavana wa kaunti
- Gavana wa kaunti anaweza kuondolewa kwa makosa makubwa, kwa kufuata mchakato uliowekwa.
Art. 181(1)
(1) Gavana wa kaunti anaweza kuondolewa kutoka afisini katika msingi wowote kati ya misingi ifuatayo- (a) ukiukaji wa katiba hii au sheria yoyote uliokithiri ; (b) ikiwa pana sababu ya kutosha kuamini kuwa gavana huyo wa kaunti amefanya uhalifu chini ya sheria ya taifa au kimataifa; (c) kutumia mamlaka ya afisi vibaya au utovu wa nidhamu uliokithiri; (d) kukosa uwezo wa kimwili au kiakili kutekeleza majukumu ya afisi ya gavana.
Soma kifungu kamili →