Art. 251
Kuondolewa afisini
- Kamishna anaweza kuondolewa kwa sababu kubwa tu, baada ya uchunguzi.
Art. 251(1)
(1) Mwanachama wa Tume (isipokuwa aliye mwanachama kutokana na wadhifa wake) , au anayeshikilia wadhifa wa afisi huru, anaweza kuondolewa afisini kwa sababu ya- (a) ukiukaji uliokithiri wa Katiba hii au sheria yoyote ikiwa ni pamoja na kuvunja sheria katika sura ya sita; (b) utovu wa nidhamu ama ni katika utendakazi wa mwanachama au yule anayeshikilia wadhifa wa afisi huru; (c) kutokuwa na uwezo wa kimwili au kiakili katika kutekeleza majukumu ya kiafisi; (d) kushindwa kufanya kazi; au (e) kufilisika.
Soma kifungu kamili →